Thursday, February 14, 2013

Historia ya Siku ya Wapendanao

Siku ya wapendanao ni sikukuu ambayo huadhimishwa kila ifikapo tarehe 14-February ya kila mwaka (Valentine Day).
Historia yake imeanzia Karne ya 3 huko Roma ambapo alikuwapo Padri Valintumis ambaye akaja kuheshimiwa kama mtakatifu hasa tarehe hiyo.

Hadithi zilizosababisha sikukuu kuenea

Inasemekana kwambaKaisari wakati huo alikuwa : yeye aliona kuwa askari mkakamavu na bora zaidi ni yule asiyeoa wala kuwa na familia (kapera). Hivyo alipiga marufuku ndoa kwa askari.
Valentinus alipinga jambo hili hivyo kuendelea kufungisha ndoa kwa siri Mfalme Claudius alipopata habari hizi aliamuru Valentinus akamatwe na kuuawa.
Kuna hadithi nyingine ya kuwa akiwa gerezani Valentinus aliandika barua ambayo ilikuwa na salamu za kwanza za Valentine kwa binti aliyekuja kumsalimia gerezani; mwisho wa barua alihitimisha kwa maneno haya: Kutoka kwa Valentinus wako.
Toka hapo Valentine anakumbukwa kama mtetezi wa wapendanao na sikukuu yake kuadhimishwa kote duniani

0 comments:

Post a Comment