MTU KWA MTU KUHUSU NGONO
“Mpenzi naomba ufanikiwe katika
mambo yote na kuwa na afya kama vile roho yako
ifanikiwavyo” 3Yohana 2. Nilipotembelea
Norhlea shule ya secondary ya wavulana huko Bulawayo, hili ndio lilikuwa fungu
la mazungumzo yangu. Wengi wa vijana wanapita na ushindi wa juu kwa makusudi ya
kufanikiwa maishani, lakini kama hawajizoezi
kuepuka uasherati hawawezi kuishi muda mrefu ili kutimiza malengo/ndoto
zao. Kuna vitisho dhahiri kwa watoto
wanaokua katika kipindi hiki cha historia.
Kuenea kwa UKIMWI kumekuwa tishio kiasi kwamba mtoa kodi wa Zimbabwe
anakatwa aslimia 3% ya mshahara wake ili kusaidia kuchangia swala la UKIMWI.
Kwa furaha ya muda mfupi, wengi wamechezea kamari furaha yao ya baadaye na
umaarufu wa maisha yao.
Kinachohitajika kwa Kijana ni kuongozwa
na kanuni kuliko msisimko. Je, Mungu ametupatia faida sisi vijana kufanya
maamuzi maishani mwetu? Mungu katika Busara yake aliumba wanaume kama viumbe
wenye akili. Hii ina maana kuwa ikiwa linaleta maana tutalifanya. Wanawake wana
hisia za haraka, kama inaonekana vema watalifanya. Haileti maana kuweka tumaini
lako katika kondomu.
Sio uungwana kumpa msichana mimba wakati hujamwoa.
Sio salama kutumaini silica yako ukiwa kwenye nchi ambayo mmoja katika kila
watu wane ana virus vya UKIMWI 1/4. Ili kuweza
kufuata kanuni kwa msimamo thabiti, inampasa kila mtu ajielewe na ajithamini.
Jifahamu wewe u nani?.
Shetani
amejaribu kutuondelea haki na uthibitisho wa kujielewa na kujifahamu nafsi zetu
tangu mwanzo. Kufahamu sisi ni akina
nani ni msingi wa kutenda kulingana na mapenzi ya Mungu na sio shetani,
“Wapenzi sasa tu wana wa Mungu.” Kwa vile Mungu ndiye mtawala wa Ulimwengu,
lazima tuwe wana wa Kifalme. Tumepangiwa mafanikio makubwa. Kila mmoja wetu
anazo angalau chembe chembe za fahamu
billion 17 kwenye ubongo wetu. Kila chembe ina uwezo wa kushughulikia aina mia
mbili za habari. Wasomi wetu wametumia sana sana 10% tu ya uwezo wa ubongo wao. Kama kipaumbele cha maisha yako ni sahihi, unaweza
kujumuishwa kwenye kundi hili dogo la wenye uwezo mkubwa wa ubongo. Shetani
amejaribu kuzuia fikara zetu ili tusiweze kufikiria chochote kiwezacho
kutufanya tufanye bidii ili kupata mafanikio ya kweli.
Fikiria! Ni
nini nitakalo ili nifanikiwe katika maisha yangu? Ni vikwazo gani vimewafanya
wengine washindwe katika kujaribu kwao? Mimi nitaviepukaje?
Katika
kugundua wewe ni nani, soma vitabu ambavyo vitakusaidia kuelewa mwenendo wa
binadamu. Biblia/Quran ndiyo vya kwanza na muhimu sana. Ndivyo vitabu pekee vinavyotoa taarifa
yenye mamlaka ya namna ilivyofanyika tukawa Hai. Watu wengi wamebadilishwa
kutoka katika tabia za kuwa wanyama au maharamia na kuwa watu wanaofanana na
Kristo/Mtume kwa kujifunza vitabu hivi. Juhudi ya roho ya kinyama haiwezi
kutawala mwanadamu ambaye anajifunza Biblia/Quran kwa dhati.
Jipe nafasi.
Watu wengi
husikiliza vitu vyote ambavyo ni kinyume vinavyozungumzwa kuwahusu na kuishia
kusema pia mambo hasi kuhusu hao wanaomsema. Wote tunayo haki tulivyo.
Tunahitaji kutambuliwa kwa mchango wetu wa namna ya pekee kwa jamii ya
binadamu. Muumini wakati mwingine hujiingiza katika ngono kabla ya ndoa kwa
sababu ya kujiona kuwa ana mwonekano hafifu. Hivi sivyo Mungu alivyotuumba,
bali mazingira yanavyotukuza.
Utafiti wa
wanasaikolojia Fulani ulionyesha kuwa, tabia ya watu kujisikia bora, kujiamini
katika mwonekano kulishuka kutoka 70% mtu akiwa na miaka mitano(5) hadi 2%
katika maisha ya awali ya utu uzima. Ni wale tu walio na elimu ya kujifahamu
wao ni akina nani na wanaojikubali wao wenyewe, watakuwa tayari kupokea na
kukabili mambo ya hasi dhidi yao.
Yusufu alipata
uzoefu mkubwa wa kukatisha tamaa wa kuuzwa utumwani, lakini alijipa nafasi ya
kuishi na ndoto zake na hatimaye akawa waziri mkuu wa Misri. Aliweza kuvumilia
majaribu ya mwanamke mrembo, ingawa ilimgharimu kwenda gerezani.
Wewe ni wa namna ya peke yako.
Bahati ya kupata
mtu mnayefanana kabisa ulimwenguni ni ndogo sana,
kama moja kwa milioni mia tatu(3ml). Una
mchango wa pekee wa kutoa katika maisha haya.
Kwanini ufe kabla
hujawakilisha mchango wako? Epuka kuzurura au kuhusiana na watu ambao
hupendezwi na viwango vya maadili yao..
Moyo wa
mwanadamu ni mnyonge, dhaifu na hauaminiki, tunavutiwa kwa nguvu zaidi na
mazungumzo ya kinyama tunayoyasikia kuliko yale ya kweli. Wakati mwingine ni
muhimu kuorodhesha mambo unayoyapenda kukuhusu wewe mwenyewe. Wakati
unapojisikia umechukizwa na kukata tamaa, chukua orodha yako na uisome kwa
sauti. Vijana wanaokwenda kwenye nyumba za ibada wana nafasi nzuri ya
kuzungukwa na vijana marafiki wanaowachangamsha. Hivyo wanafikiria zaidi kuhusu
masuala ya uzalishaji. Jipatie nafasi..
Acha ndoto zako zitimie.
Uwe na lengo maishani.
Kuishi maisha
yasiyo na malengo maalum ni hasara na kuishi kusikofaa. Kila mtu inampasa awe
na kusudi maalum la wazi maishani mwake. Kama
hujui unachotaka kufanya na maisha yako, tafuta washauri wenye busara kuliko
wewe wakusaidie. Maisha bila lengo hushusha hadhi zetu na kutufanya tusiwe na
tofauti na wanyama. Sishangai watu wengi wana tabia kama za wanyama, wakitawaliwa
na tamaa zao.
Ondoa Giza.
Thomas Edson
alipokuwa anagundua mwanga wa balbu, hakuna ambacho kingemzuia kufanya hivyo.
Mama yake aliambiwa na mkuu wa shule kwamba hatafanikiwa sana na mara kwa mara alimruhusu akauze
magazeti. Magazeti haya yalikuwa na taarifa za ugunduzi wa karibuni na hivyo
zikajenga katika moyo wa Thomas shauku ya kugundua kitu Fulani. Usiku aliweza
kwenda maabara kufanya jaribio moja baada ya jingine. Baada ya majaribio mengi
mama yake alijaribu kumkatisha tamaa kwa kusema alikuwa anapoteza muda. Hata
hivyo Thomas alimjibu kwamba japo hadi wakati alikuwa hajafanikiwa, lakini moja
ya jaribio litafanikiwa kwa hakika. Muda mfupi baada ya hapo, Thomas Edson
akagundua mwanga wa balbu
Lengo ni kitu
ambacho kinakuchochea kuwa na ari ya juu kiasi kwamba hata mama yako hawezi
kukuzuia kukifanya, Watu wengi wamefanya majaribio kulewa, Madawa ya kulevya na
ngono, na vyote hivi havikuwaletea furaha ya kudumu. Una bahati na faida ya
kuelewa ni majaribio gani hayafanikiwi. Kwa nini ufanye uchaguzi wa
kipumbavu…..!!!
Wenye busara
hujisahihisha wenyewe kutokana na makosa ya kipumbavu waliyoyatenda.
Lenga mbali.
Lengo kuu ambalo
kila Mwanadamu anahitaji kulifanya katika maisha ni kuongozwa na kanuni na sio
hisia. “Kusalimisha uwezo wetu wote kwa Mungu hupunguza sana matatizo ya maisha.” Inadhoofisha na
kufupisha maelfu ya masumbufu na tamaa za asili za moyo.” Messages to young
Lovers”. UK.
63, Ellen White
Tamaa za asili za moyo:
Kando ya kujizuia kufanya ngono na
wasichana, kijana wa kiume akubaliane na matukio machache ambayo yamekuwa wazi.
Wakati wa kuandaa kuandika makala hii, kijana mmoja kutoka shule ya sekondari
aliniomba nijumuishe habari kuhusu ubasha au ushoga na punyeto.
Ubasha na Ushoga.
Wazimbabwe
wengi hawafikirii hili kuwa tatizo kubwa, hivyo utafiti kidogo sana umefanywa
kuhusiana na swala hili. Kwanza hebu tuweke wazi misimamo yetu, tunaamini
kwamba ubasha au ushoga umelaaniwa katika Biblia Yuda anaelezea hili kuwa moja
ya sababu kwa nini Mungu aliadhibu Sodoma na Gomora. Yuda 7:8, Paulo alikiita
kitendo hiki kuwa sio cha kawaida na alikilinganisha na kiumbe badala ya Mungu.
Hata Rais Mugabe amekemea na amelaani kitendo hiki kwa kusema kwamba sio cha Kibiblia
au kiafrika. Kwa mara ya kwanza nilipokutana na matendo ya ubasha na ushoga
ilikuwa kwenye shule ya misheni kama kilometa 28 nje ya Harare. Mkuu wa Bweni wa shule hii alikuwa
anawapanga wavulana mstarini na kuchagua wote waliokuwa na mwonekano wa sura
nzuri. Baada ya hapo aliwapangia kufanya kazi nyumbani kwake. Kuna wakati
mwingine aliwabusu hawa wavulana na huenda hata kulawiti. Alikuwa ameoa
mwanamke jeuri na anayemtawala kiasi kwamba wakati mwingine alimpiga mumewe.
Nadharia nyingi
zimeendelea kuelezea kwa nini watu wngine wamechagua uhusiano wa ngono ya
ubasha au ushoga kuliko ule wa mke na mume. Katika utafiti wangu nimetambua
kwamba wengi wa mabasha au mashoga watakuwa hivyo kutokana na uhusiano wao na
rafiki wanayemwamini, kiongozi au jamaa. Hata katika nchi zinazovumilia mambo
kama haya kama ulaya, ubasha au ushoga
haufikiriwi kuwa sahihi kwa 66% ya wanaume na 50% ya wanawake. Huko Zimbabwe
99% ya watu wanauona Ubasha au ushoga ni mbaya. Uhusiano wa kulawitiana kwa
wanaume unasemekana kuwa na maumivu na uchungu, lakini wengi wanaendelea na
hivyo kwa vile wanasisimuana hadi kufikia mshindo. Baadhi ya mabasha au
mashoga, wanapenda kuwa na uhusiano wa ngono wa kawaida kati ya mke na mume.
Unakuta wana mke na watoto, lakini bado wanapendelea kufanya ngono na wanaume
wengine. Magonjwa ya UKIMWI na Heapatitis B ni tishio la afya kwa mabasha na
mashoga.
Punyeto.
Unakumbuka kuota
kuhusu picha au sinema ya ngono halafu unakakamaa kabla hujajua kuwa nguo yako
ya ndani imelowana? Vijana wengi hupitia
uzoefu huu. Mamlaka ya Australia
inaamini kuwa hadi 90% ya wavulana wanapitia uzoefu katika maisha yao, na 10%
wanaosema hawakupitia ni waongo. Je, ndoto nyevu zinatokeaje? Wakati homoni au
vichocheo vinapotolewa, mbegu za kiume hujaza ndani ya mirija ya kiume (seminal
vesicles). Mirija hii ikijaa, mwili hujaribu kuzitoa na njia ya kawaida ya
kuzitoa ni kwa njia ya ndoto nyevu.
Hii yenyewe sio
kosa kwa vile ni hatua ya Kibayologia, lakini inaweza kujenga tabia ambayo ina
madhara na ni dhambi kwa Mungu. Punyeto au ngono binafsi hudhihirisha udhaifu
kwa kijana ambaye hufinyafinya, hushikashika au kuchezea viungo vyake vya kiume
ili kujitimizia haja ya ngono na kufikia mshindo. Hii sio kitu kinachofanyika
bila mtu kuwa na fahamu bali hufanyika mtu akiwa na fahamu kamili. Punyeto ina madhara kwa vile inawashawishi
vijana kutafakari kuhusu ngono na kuondoa mawazo ya kutafakari kuhusu mambo
mengine muhimu. Kazi za shule zitaathirika
kwa mazoea haya.
P.E
Tatizo kubwa la
punyeto ni kutoa mbegu za kiume kabla ya kufikia mshindo. Watu wengi huchukua
hata dakika kumi(10) kabla ya kutoa mbegu za kiume wakiwa wanatenda tendo la
ngono, lakini katika hali ya punyeto mbegu za kiume hutoka kabla ya mshindo
sekunde chache baada ya kitendo kuanza.
Wanawake wengi hawawezi kuvumilia hali ya aina hii mpaka kifo
kiwatenganishe wakiwa pamoja. Kila mmoja
ana haki kwa mwenzake kumfanikisha katika tendo hili, hivyo usimkatalie mwenzi
wako wa baadaye kile ambacho anapaswa kukipata kwako. Kufanya mapenzi na mtu wa
jinsia yako sio kawaida kwa namna yoyote.
Kwa hitimisho,
napenda kusema kwamba Mungu alituumba kwa namna ya ajabu na hivyo tunatakiwa
kumcha kwa kicho. Kama tukifuata mashauri ndani ya maandiko yake katika maisha
yetu hatutabadilishwa kirahisi. Ngono si kitu cha kuchangamkia. Kwa wastani
waliooana wana miaka arobaini ya kufanyisha viungo vyao vya uzazi mazoezi haya.
Kuharakisha zawadi hii, kunaweza kukupunguzia nafasi ya bahati yako njema.
Uvumilivu ni maadili na jambo la msingi.
Created
by Michael Nyagei Magessa
Thank you! Article imesimama
ReplyDeleteAhsante sana 🙏🙏
DeleteNadhani kwa sasa huna tena haya madini
ReplyDelete