MAUMIVU YA KICHWA
Maumivu ya kichwa hutokea watu wengi sana wa umri wote. Ni dalili inayopelekea watu wengi kwenda hospitali kwa ajili ya matibabu. Kuna sababu nyingi zinazosababisha maumivu ya kichwa. Nyingi zikiwa zisizohatarisha maisha ya mtu, na baadhi zikiwa hatari kwa uhai wa mtu. Maumivu ya kichwa yanaweza kuwa ya kuanza mara moja ghafla (acute headache) au maumivu ya muda mrefu yanayokuja na kuacha (chronic headache).
Dalili ambazo zinaweza kuambatana na maumivu ya kichwa ni homa, kutapika, kizunguzungu, moyo kwenda mbio, kupoteza fahamu, kutoona vizuri, kupata degedege na nyingine.
Kwa kawaida unapopata maumivu ya kichwa onana na daktari wako kwa matibabu. Ikiwa maumivu ya kichwa yanaambatana na dalili zifuatazo basi wahi haraka sana hospitali iliyo karibu na wewe. Kuona vitu viwili viwili au giza, kupata degedege (convulsions), kupoteza fahamu, kutapika sana na moyo kwenda mbio.
Sababu za Maumivu ya Kichwa
• Malaria
• Ajali ya kichwa
• Matatizo ya macho
• Damu kuvuja kwenye ubongo
• Shinikizo la damu la kupanda
• Uvimbe kwenye ubongo
• Upungufu wa damu
• Upungufu wa maji mwilini
• Kifafa
Magonjwa ya kuambukiza kama;
• Malaria
• Homa ya uti wa mgongo
• Homa ya tumbo
• Ugonjwa wa toxoplasmosis
Vipimo
Vipimo vinavyofanyika kutokana na maumivu ya kichwa hutegemea na chanzo chake. Vipimo hivi husaidia kugundua chanzo cha maumivu ya kichwa ili yatibiwe. Baadhi ya vipimo vifuatavyo vinaweza kufanyika.
Kipimo cha damu cha malaria au homa ya tumbo (typhoid)Wingi wa damu (haemoglobin concentration)Kipimo cha maji ya mgongo (Lumbar puncture)X-ray ya kichwaCT Scan ya kichwaMRI ya kichwa
Matibabu
Maumivu ya kichwa hutibiwa na kuisha pale ambapo chanzo chake kimejulikana na kudhibitiwa. Pale ambapo chanzo hakijajulikana, dawa za kutuliza maumivu hupunguza ukali lakini baadae yanaweza kujiridua tena. Dawa za NSAID kama Diclofenac na paracetamol hutumika kutuliza maumivu huku matibabu mengine yakiendelea. Kwa baadhi ya hali zinazosababisha maumivu ya kichwa huitaji matibabu yanayoweza kuhusisha upasuaji.
Wakati mwingine maumivu ya kichwa yanaweza kutokana na msongo wa mawazo, uchovu wa mwili na mambo mengi ya maisha. kwa kuzingatia yafuatayo:
Kunywa maji mengi kila siku, zisipungue lita 2.5 au glasi 10 kwa siku moja. Itakusaidia kupunguza uchafu mwilini na ubongo upate damu ya kutosha.Kufanya mazoezi kila siku angalau kwa nusu saa. Huimarisha kinga ya mwili wako, mzunguko wa damu na ukakamavu.Kupata mlo wenye virutubisho vya kutosha.Pata muda wa kupumzika wa kutosha, angalau masaa 8 ya kulala wakati wa usiku.Pata muda wa kutulia na kutafakari kuhusu maisha yako, kupanga mipango yako na kutuliza nafsi yako.Pata muda wa kuwa na rafiki zako, ndugu na jamaa unaowapenda
0 comments:
Post a Comment