Kwa ufupi
- Taasisi ya Taifa ya Afya ya nchini Marekani (NIH) inaeleza kwamba sababu za jumla za ugumba ni umri na asilimia nne ya wanaume wenye umri wa miaka 50 na kuendelea wanaweza kuwa na tatizo hilo wakati nusu ya wanaume wenye umri wa miaka 75 wanakumbwa na ugumba.
Ukosefu wa nguvu za kiume nchini twaweza kusema ni janga. Hii
ni kutokana na tafiti zilizowahi kufanywa na pia kuzagaa kwa vibao vya
matangazo kuhusu dawa au tiba ya tatizo hilo.
Tatizo hili halipo kwa wazee kama ilivyodhaniwa zamani, bali hata kwa vijana, wake kwa waume wamekuwa wakiguswa na tatizo hilo.
Sababu nyingi zimewahi kuanishwa kuchochea ugumba
kwa wanaume ikiwamo maradhi, kutazama luninga kwa muda mrefu na
kutofanya mazoezi.
Hivi karibuni wataalamu katika Jarida la Jinsia na
Tiba la nchini Uingereza, lililochapishwa Januari lilieleza sababu kuu
duniani zinazochochea ugumba kwa wanaume iwe wa muda mrefu au wa
kudumu.
Taasisi ya Taifa ya Afya ya nchini Marekani (NIH)
inaeleza kwamba sababu za jumla za ugumba ni umri na asilimia nne ya
wanaume wenye umri wa miaka 50 na kuendelea wanaweza kuwa na tatizo
hilo wakati nusu ya wanaume wenye umri wa miaka 75 wanakumbwa na ugumba.
Daktari wa Upasuaji na Nguvu za Kiume katika Chuo
Kikuu cha Tiba cha Maryland, Dk Andrew Kramer anasema karibu nusu ya
wanawake na wanaume wote duniani wanakosa nguvu za kiume aidha moja kwa
moja au katika nyakati fulani za maisha yao.
Madereva
Dk Kava anasema wakati wa zama za chuma ilibainika
kwamba wanaume wanaoendesha baiskeli kwa muda mrefu, waendesha farasi
na madereva wa magari kwa muda mrefu wamo hatarini kukosa nguvu za
kiume.
Jarida la tiba lilifanya utafiti na kubaini kuwa
asilimia nne ya wanaume wanaoendesha baiskeli kwa saa tatu au zaidi kwa
wiki wanapata matatizo ya nguvu za kiume.
Anasema unapokaa kwenye gari, farasi au baiskeli
kwa muda mmrefu unaweka nguvu katika neva na mishipa midogo inayobeba
damu kwenda katika uume.
Anafafanua kwamba uendeshaji wa vyombo hivyo kwa muda mrefu unaharibu mishipa midogo na damu haiendi inavyotakiwa katika uume.
Maradhi ya fizi
Maradhi ya fizi
Pengine unaweza kujiuliza fizi na nguvu za kiume vina uhusiano
gani? Wataalamu wa Afya wanasema, kuwa na matatizo sugu ya fizi au fizi
zilizoathirika kunaweza kuongeza hatari ya mtu kukosa nguvu za kiume.
Watafiti wanasema maradhi ya fizi ni dalili za
afya dhaifu na inahusishwa na ongezeko la maradhi ya moyo na upungufu wa
nguvu a kiume.
“Maradhi ya fizi yanaweza kusababisha matatizo
katika kusukuma damu, hivyo matatizo hayo yakizidi, yanaweza kusababisha
damu ishindwe kufika katika uume,” anasema Bruce Kava, Mwenyekiti wa
Tiba ya Mfumo wa Mkojo katika Chuo Kikuu cha Tiba cha Miami Miller.
Kisukari ni sababu nyingine na Taasisi ya Taifa ya
Afya ya nchini Marekani inasema wanaume wanaougua maradhi ya kisukari
wana hatari mara tatu zaidi kukosa nguvu za kiume kuliko wanaume wasio
na maradhi hayo.
Dk Kramer anasema sukari isipodhibitiwa katika damu, inaharibu neva na misuli midogo inayodhibiti kusimama kwa uume.
Pia asilimia 61 ya watu wenye msongo wa mawazo hawawezi kuwa na nguvu za kiume.
Taarifa kutoka Kliniki ya Cleveland inaeleza
kwamba msongo wa mawazo unasababisha mambo makubwa zaidi katika mwili na
unaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa nguvu za kiume.
Msongo wa mawazo unasababisha Kemikali za seli za
ubongo zinazowasiliana katika kusisimua mtiririko wa damu hadi katika
uume kushindwa kufanya kazi.
Pia Dk Malebo anasema wanaume hukosa nguvu za
kiume kutokana na msongo wa mawazo ambao unatokana na migogoro ya
kifamilia, ufukara au imani za kishirikina.
Dk Kramer anasema dawa za saratani na zile za
kuondoa vipara zinazotumiwa zaidi na wanaume zinaweza kusababisha
madhara ya nguvu za kiume.
Mkuu wa Kitengo cha Utafiti wa Tiba Asilia katika
taasisi ya utafiti wa tiba nchini (NIMR), Dk Hamis Malebo anasema
sababu kuu za ugumba kwa Tanzania ni mfumo wa maisha.
Anafafanua kwamba aina za vyakula, mtindo wa
maisha, msongo wa mawazo na utofauti katika vichocheo ni baadhi tu ya
sababu za ukosefu wa nguvu za kiume.
“Baadhi ya vyakula vina kemikali ambazo zinapoingia katika mwili
zinaharibu usukumwaji wa damu katika uume” anasema dk malebo ambaye
aliwahi kufanya utafiti kuhusu ugumba.
Samaki na maziwa ni sababu
Kwa mfano, watu wengi hununua maziwa ya ng’ombe ambayo yamechomwa sindano siku mbili au moja nyuma bila wao kufahamu
“Au samaki wanaovuliwa kwa kemikali na mabomu ni sababu zinazochangia kwa kiasi kikubwa ukosefu wa nguvu za kiume,” anasema.
Anasema kemikali hizo zinaathiri uzalishaji wa vichocheo na usukumwaji wa damu kutoka katika moyo hadi katika uume.
Anashauri kuwa ili kuepukana na tatizo la nguvu
za kiume hasa kwa wale wenye msongo wa mawazo sulushisho ni kubadili
mfumo wa maisha.
“Kuhusu mvurugiko wa homoni, udhibiti wa serikali
unahitajika. Maziwa ya ng’ombe, yanayokamuliwa wakati ng’ombe amechomwa
sindano pamoja kemikali za kuvulia samaki zidhibitiwe,” anasema.
Anasema uwiano mbovu wa vichocheo unaweza kutibika hospitali kwa dawa zinazorekebisha mfumo huo na pia zipo dawa za asili.
Mmea wa Alikisusi (licorice) kwa kisayansi
Glycyrrhiza Giabra una uwezo wa kutengeneza uwiano wa vichocheo kwa
wanaume wenye matatizo ya nguvu za kiume.
0 comments:
Post a Comment