Friday, February 15, 2013

Papa (Samaki)

Papa ni kundi la spishi 500 za samaki wenye kiunzi cha gegedu badala ya mifupa. Gegedu ni dutu ya kunyambulika kama mpira mgumu lakini laini kuliko mifupa kamili. Karibu spishi zote wanaishi katika maji ya chumvi baharini.
Papa wengi ni wavindaji wanaokula samaki na wanyama wengine wa baharini. Spishi kadhaa wanahofiwa kwa sababu kushika wanadamu. Lakini papa wakubwa sana wanakula planktoni kama nyangumi wakubwa.
Papa mkubwa kabisa ni papa nyangumi (rhincodon typus) anayefikia urefu wa mita 14 na uzito wa tani 12 ambaye ni pia samaki mkubwa duniani anakula planktoni. Spishi ndogo ni Etmopterus perryi yenye urefu wa sentimita 17 tu.
Spishi nyingi za papa ziko hatarini ya kupotea kwa sababu wanavindwa mno.
Papa huwa na meno mengi yanayoendelea kukua muda wote wa maisha yake mstari baada ya mstari wa meno yanayoanza kukua nyuma ya meno ya nje na kuchukua nafasi yao mfululizo.
Wana uwezo mkubwa wa kunusu ndani ya maji hasa damu ya kiumbe aliyeumizwa kwenye umbali wa kilomita. Kupitia ngozi wanatambua pia mwendo ndani ya maji na wanaelekea penye chanzo cha mwendo.
Spishi nne wametambuliwa kuwa ni hatari kwa wanadamu. Lakini jumla ya ajali ambako mwanadamu anang'atwa na papa ni takriban 100 kwa mwaka kote duniani; mara nyingi watu wanajeruhiwa na mwaka 2007 kuna ya kifo kimoja kutokana na papa. Wataalamu wanajadiliana kama papa wanashambulia kweli au kama wanjisikia mara nyingi wameshambuliwa na watu wanaowakaribia mno au kama papa anamchanganya mwanadamu na windo la kawaida.
Kinyume chake kuna papa milioni 200 wanaouawa kila mwaka na wanadamu.

Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Chondrichthyes (Samaki wenye gegedu)
Nusungeli: Elasmobranchii (Papa na taa)
Oda ya juu: Selachimorpha (Papa)

0 comments:

Post a Comment