Saturday, April 23, 2016

UGONJWA WA KIHARUSI: DALILI, SABABU NA VIPIMO


Kiharusi ni ugonjwa ambao huathiri ubongo na ufanyaji kazi wake. Hujulikana kama stroke au brain attack kwa Kiingereza. Unapopata kiharusi, seli za sehemu fulani za ubongo hushidwa kufanya kazi kutokana na damu kushindwa kufika kwenye seli hizo za ubongo. Kiharusi huweza kuathiri sehemu yoyote ya ubongo, na hivyo kuathiri ufanyaji wa shughuli za kila siku za mgonjwa.
Ugonjwa huu ni hatari na mara nyingi hujitokeza ghafla, ingawa wakati mwingine kuna dalili unazoweza kupata kuashiria ugonjwa huu. Dalili hutegemea na sehemu ya ubongo iliyoathirika. Sehemu kubwa ya ubongo ikiathirika huweza kusababisha mtu kushindwa kuongea, kujitambua na wengi hushindwa kurudi hali zao za kawaida.
Huu ni ugonjwa hatari ambao unaweza kusababisha mtu kupoteza maisha ghafla. Hivyo ni muhimu sana kuwahi hospitali kwa ajili ya matibabu. Pamoja na matibabu mazuri, kuna uwezekano mgonjwa akapata ulemavu wa maisha kutokana na kiharusi. Uwezekano wa kupata kiharusi huongezeka kadri umri unavyoenda.

Namna Kiharusi Kinavyotokea

Ili kufanya kazi zake, seli za kwenye ubongo hutegemea kupata virutubisho na oksijeni kutoka kwenye damu. Kukosa damu hata kwa dakika moja, huathiri kwa kiasi kikubwa uafanyaji kazi huu. Seli hizi zinaweza kufa kabisa kama zikikosa damu kwa dakika 5, na huwa haziwezi kutengeneza seli mpya.
Kwa hiyo pale inapotokea mshipa wa damu wa sehemu fulani ya ubongo umeziba au kupasuka, damu hushindwa kufika kwenye sehemu hiyo na hivyo seli zake zitashindwa kufanya kazi vizuri. Hali hii ikiendelea zaidi, seli hizo zitakufa kabisa. Kila sehemu ya ubongo huratibu kazi maalumu mwilini, mfano kuongea. Seli zinazoratibu kazi fulani zinapokufa, kazi hizo hushindwa kufanyika tena na hivyo dalili za kiharusi hujitokeza ikitegemea na sehemu ya ubongo iliyoathiirika.

Kuna aina mbili za kiharusi:

Kiharusi kutokana na mishipa ya damu kuziba kwenye ubongo (ischemic stroke)
kiharusi kutokana na mishipa ya damu kupasuka kwenye ubongo (hemorrhagic stroke)
Mishipa ya damu kuziba kwenye ubongo
(ischemic stroke) ni aina ya kiharusi kinachojitokeza zaidi kwa kiasi cha silimia 80, asilimia nyingine hutokana na mishipa ya damu kupasuka.

Dalili Za Kiharusi

Ugonjwa huu unaweza kujitokeza haraka na ghafla bila kutarajia. Na dalili hizi zinaweza kutokea kwenye sehemu yoyote ya mwili. Unapopata kiharusi unaweza kupata dalili zifuatazo:
Kushindwa kuongea au kuelewa. Unaweza kupatwa na hali ya kuchanganyikiwa, kushindwa kuongea ua kuelewa ghafla.
Kukosa nguvu au ganzi upande mmoja wa mwili. Ghafla tu unaweza kupatwa na hali ya kukosa nguvu, ganzi kwenye uso, mkono au mguu, hasa upande mmoja wa mwili. Mdomo kuelekea upande mmoja unapocheka, kushindwa kunyanyua mkono upande mmoja.
Kushindwa kuona vizuri. Hali ya kushindwa kuona vizuri inaweza kujitokeza ghafla. Inaweza kuwa kwa macho yote au jicho moja tu.
Kushindwa kutembea. Ghafla tu unaweza kushindwa kutembea kutokana na kupata kizunguzungu kikali, kukosa uwiano kwa ghafla.
Maumivu makali ya kichwa ghafla.
Dalili nyingine ambazo unaweza kupata ni kupoteza fahamu, degedege (convulsions) , kushindwa kula, kushindwa kuzuia choo.
Kiharusi ni ugonjwa unaohitaji matibabu haraka sana. Kadri mgonjwa anapozidi kuchelewa kupata mtibabu ndivyo seli za ubongo zinavyozidi kufa. Kufa kwa seli hizi kutasababisha ulemavu kwa mgonjwa.

Sababu Hatarishi Za Kiharusi Kutokea

Vitu au tabia zifuatazo huongeza hatari ya kiharusi kutokea kwako:
Shinikizo la Damu La Kupanda
Uvutaji sigara
Magonjwa ya moyo
Magonjwa kama Kisukari
Kiwangi kikubwa cha lehemu kwenye damu
Kutofanya mazoezi
Uzito mkubwa
Unywaji wa pombe kiholela
Vipimo
Unapopata tatizo hili unaweza kufanyiwa vipimo vifuatavyo ili kujua aina ya kiharusi ili upate matibabau sahihi.
Vipimo Vya Damu:
Complete Blood Count
Clotting factors
Kipimo cha CT Scan ya Ubongo
Kipimo cha MRI ya Ubongo

Kujikinga Na Kiharusi

Kujikinga usipate kiharusi ni kitu muhimu sana, kwani hauwezi kujua kikitokea kitakuathiri namna gani. Kuna tabia hatarishi nyingi ambazo unaweza kuziondoa ka kufanya mabadiliko fulani katika maisha yako kama tutakavyoona hapo chini.
Acha kuvuta sigara.
Shinikizo la damu la kupanda
(hypertension) . Fanya mazoezi, kula mlo kamili, dhibiti uzito,punguza chumvi na tumia dawa kudhibiti presha.
Kisukari.
Magonjwa ya moyo.
Fanya Mazoezi.
Dhibiti Uzito Wako.

LEHEMU NA HATARI YA MAGONJWA YA MOYO NA MISHIPA YA DAMU


Lehemu hujulikana kama cholesterol kwa Kiingereza. Ni aina ya mafuta ambayo ni sehemu muhimu ya ufanyaji kazi wa mwili wa binadamu. Lehemu hubebwa kwenye damu na aina ya protini iitwayo lipoprotini. Kutokana na uzito wa protini hizi kuna Low Density Lipoprotein (LDL) na
High Density Lipoprotein (HDL) . Kati ya hizi HDL ni lehemu nzuri na LDL ni lehemu mbaya.

LEHEMU INAVYOATHIRI MWILI

Kiasi cha lehemu ya kwenye damu kinapoongezeka na kuwa juu, huongeza hatari ya magonjwa ya moyo kama shambulio la moyo, shinikizo la damu na magonjwa mengine kama kiharusi. Aina ya lehemu ambayo huathiri mwili vibaya ni LDL au Low Density Lipoprotein , hii inapoongezeka sana ndio huongeza hatari ya magonjwa haya.
Lehemu ya LDL inapoongezeka sana kwenye damu, hujikusanya ndani ya mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye moyo na ubongo. Kadri inavyozidi kujikusanya ndipo inavyopunguza tundu la mishipa ya damu. Hali hii huitwa
atherosclerosis kwa kitaalamu. Inapotokea damu imeganda basi huziba sehemu ya mshipa lehemu ilipo jikusanya na hivyo shambulio la moyo au kiharusi hutokea.

NJIA ZA KUPUNGUZA LEHEMU MWILINI

Kudhibiti kiasi cha lehemu mwilini mwako ni sehemu muhimu sana ya kukabiliana na hatari ya kupata magonjwa ya moyo na mishipa ya damu. Unaweza ukazingatia yafuatayo kukusaidia kufanikisha hili.
Fanya mlo wako uwe na mboga za majani, matunda, nafaka zisizokobolewa, mafuta ya mimea na nyama nyeupe zisizo na mafuta.
Fanya mazoezi ya mwili. Pata angalau nusu saa kwa siku kukimbia, kuruka kamba, kuendesha baiskeli, kuogelea, kutembea haraka, kucheza au vingine unavyopenda kufanya ili mradi umuvike na utoe jasho!
Usivute Sigara

DONDOO ZA LISHE WAKATI WA UJAUZITO


Unakula nini wakati wa ujauzito? Lishe wakati wa ujauzito ni muhimu kwa ajili ya afya yako na maendeleo mazuri ya mtoto anayekua tumboni. Zifuatazo ni dondoo za kukuwezesha uwe na lishe nzuri wakati wa ujauzito:

Jitahidi upate mlo kamili kila siku kwa kupata vyakula vya wanga, protini, mafuta, vitamini, madini na maji ya kutosha.
Fanya nusu ya mlo wako uwe ni mchanganyiko wa matunda na mboga za majani.
mjazito akipata mlo wenye mgoga za
mjazito akipata mlo wenye mgoga za majani
Tumia nafaka zisizokobolewa kama unga wa dona au mtama, mchele usiokobolewa, mikate ya brown au whole grain cereals.
Tumia maziwa yenye fafi kidogo( skimmed milk) au maziwa na vinywaji vya soya.
Chagua vyanzo vyako vya protini zaidi katika samaki, kuku, mayai, jamii ya maharage, soya na karanga.
Tumia zaidi mafuta ya mimea katika mapishi yako kama mafuta ya alizeti, pamba au mizeituni (Olive oil).
mafuta ya alizeti
mafuta ya alizeti
Punguza vyakula vyenye sukari za kuongeza (hasa artificial sugars) na mafuta kama biskuti, pipi, soft drinks, soda, pipi, ice creams, vyakula vya kukaanga na hot dogs.
Kunywa maji mengi, zisipungue lita 2.5 kwa siku.
Mazoezi mepesi kama kutembea kwa dakika 30 kwa siku.
Epuka matumizi ya pombe kwani yataathiri afya ya mtoto wako.
usinywe pombe.
Tumia virutubisho ziada (supplements) utakazopata kliniki.

Tuesday, April 12, 2016

HUYU NDIYO EDWARD MORINGE SOKOINE SHUJAA MZALEND WA TANGANYIKA,ADUI WA WAHUJUMU UCHUMI NA WATENDAJI WAZEMBE1/8/1938 -12/4/1984

"Ole wao wale wanaotumia nafasi zao za umma na serikali,kuiba,kuhujumu uchumi,kupokea rushwa,maana salama yao ni kudra za Mwenyezi Mungu labda nisiwajue"
Hayo ni maneno aliyowahi kuyatamka hayati kaka na mzalendo wa taifa hili shujaa Moringe Sokoine,wakati akilihutubia kwenye mkutano kikao cha NEC mjini Dodoma 12/04/1984,takribani miaka 30 iliyopita,wakati huo vita ya kupambana na suala la uzembe makazini,ulangunguzi,rushwa na biashara ya magendo,enzi hizo taifa lilikuwa la moto kila sehemu ilikuwa moto,lakini mpaka leo kauli yake inaishi,inatumika,inaamsha hali ya uzalendo na maadili ya taifa hasa wakati huu ambapo wanasiasa na serikali kwa ujumla wanaishi kinyume na misingi mikuu ya taifa hili,misingi mikuu ya chama chao na msingi mkuu wa uwajibikaji wa serikali,leo tunamkumbuka,tunakumbuka kifo cha mpendwa wetu huyo kwa yale mazuri aliyoifanyia Tanganyika kwa ujumla wake,lakini pindi tunakumbuka kumbukumbu hii tujiulize je?utakapofariki utakumbukwa kwa lipi?je viongozi wetu wanaishi kimatendo kma hayati wetu Sokoine?
ALIPOTOKA MH SOKOINE NA SAFARI YAKE NDEFU KUELEKEA KULETA TANGANYIKA TUITAKAYO.
Hayati Sokoine alizaliwa mnamo mwaka 1/8/1938 katika wilaya ya MAASAI LAND ambayo kwa sasa inafahamika kama wilaya ya Monduli,wilaya iliyoko mkoani Arusha,hayati Sokoine alipata elimu yake ya msingi Monduli,akafaulu kujiunga na shule ya sekondari Umbwe,hii ilikuwa ni kuanzia mwaka 1948 mpaka 1958,alipomaliza hapo alijiunga rasmi na chama cha TANU 1961,kisha alipata nafasi ya kwenda nchini Ujerumani mwaka 1962 mpaka 1963 kusomea mambo ya uongozi na utawala na aliporudi akateuliwa kuwa afisa mtendaji wilaya ya Maasai Land,na kutiokana na ufanyakazi wake uliotukuka wilayani Monduli wananchi hawakuwa na budi kumchagua kuwa mwakilishi wao bungeni yaani mbunge wa Monduli na ufanisi wake kiutendaji ulionekana machoni mwa watendaji wakuu wa serikali na hayati baba wa taifa Nyerere na akachaguliwa kuwa Naibu wa wizara ya mawasiliano na Usafiri hii ilikuwa mwaka 1967,kama hiyo haitoshi nyota ya kiuongozi ilizidi kumwangazia ambapo mwaka 1972 aliteuliwa kuwa waziri wa Usalama na hatimaye mwaka 1977 aliteuliwa rasmi kuwa waziri mukuu wa iliyokuwa serikali ya Tanganyika,na Muungano wa Tanzania,
Hayati sokoine alikuwa hasa mzalendo na aliependa siasa za ujamaa na hata kupelekea kumwomba baba wa taifa ruhusa ya kusisimama kwa mda kama waziri mkuu ili aende kusomea zaidi mambo ya ujamaa nchi za nje,hii ilikuwa mwaka 1981,1983 alirudi kuendelea kama waziri mkuu kuanzia wa Tanzania mpaka siku ya tarehe 12/4/1984 alipopata ajali mbaya ya kugongwa na gari lililokuwa likiendeshwa na mkimbizi wa kisiasa kutoka nchini Afrika kusini aliyejulikana zaidi kwa jina la Dube,eneo la Wami Dakawa sasa Wami Sokoine mkoani Mororgoro,ajali iliyopelekea mauti yake palepale,kifo ambacho mpaka leo kinaacha maswali mengi na kwa bahati mbaya hakuna hata mwandishi mmoja aliefanya mahojiano na bwana Dube ambaye kwa sasa yupo nchini Afrika kusini anakula bata,,
UTATA WA KIFO CHAKE NA MASWALI MAGUMU YASIYOJIBIKA KIRAHISI
Itakumbukwa kwamba karibia viongozi wakubwa wote wa serikali waliondoka mjini Dodoma kwa ndege mara baada ya kikao cha NEC,Isipokuwa hayati Sokoine ,yeye alisema wazi ni muumini wa sera ya kilimo ni uti wa mgongo wa taifa,hivyo alipendekeza kusafiri kwa njia ya barabara ili ajionee Mashamba makubwa na maendeleo ya kilimo kwa ujumla,
2:Gari lililomgonga liliwezaje kupenya magari yote yaliyokuwa kwenye msafara wa waziri mkuu Sokoine mpaka kulifikia gari la marehemu Sokoine na kuligonga?vp trafiki walikuwa wapi mpaka lori hilo limfikie kiongozi huyo?vipi maafisa wa ulinzi ambao kazi yao ni kumlinda?
3:Katika ajali hiyo aliyefariki ni hayati Sokoine pekee,vpi kuhusu wengine kwani hakuna hata aliyejeruhiwa pakubwa
4:Aliyesababisha ajali hiyo alikuja kuachiwa huru na akarudishwa kwao A,kusini,
TETESI JUU YA UTATA WA KIFO CHAKE
Ni ukweli kwamba ukiwa kiongozi unaetimiza majukumu yako kikamilifu ni lazima utakuwa na maadui wengi na wanaokutafta kwa kila namna,hayati sokoine kutokana na vita yake dhidi ya Wahujumu uchumi,mtakumbuka wakati wa vita hiyo kuna watu walienda kuficha bidhaa mapolini na wengine kumwaga mitoni,baharini na ziwani,hali ilikuwa tete kwa wahujumu uchumi pia Walanguzi,wazee wa Magendo,wala rushwa na watendaji wazembe wa serikilini,na hapa anatajwa mzee Kawawa kuwa alikuwa miongoni mwa watu waliokemewa na maremu wakati wa kikao hicho cha mwisho mjini Dodoma,
Pia inadaiwa aliiva katika misingi ya kijamaa kupita kiasi,hali ambayo ilimtisha hata baba wa taifa
Je ni ajali ya kawaida iliyotokana na mikono na mapenzi ya Mungu?ama mkono wa binadamu?swali hili ni gumu na lina dead end
MCHANGO WAKE KWA TAIFA NA MISIMAMO NA MITAZAMO YAKE
1:Aliamini katika Haki,Usawa na uwajibikaji
2:Aliamini katika siasa za ujamaa zaidi ya siasa yeyote ile.
3:Aliamini kwamba maendeleo huja kwa watu kujituma kufanya kazi halali na bidii.
4:Aliamini katika mabadiliko chanya
5:Alikuwa mzalendo hasa kwa taifa hili
6:Aliichukia vitendo vya rushwa,hujuma,uhujumu uchumi,ulanguzi na magendo.
7:Alikuwa mtu wa vitendo na kamwe alikuwa si mtu wa kupenda kulalamikalalamika.
MCHANGO WAKE KITAIFA
1:Alikuwa mstari wa mbele enzi za vita ya Kagera pindi tunampiga Nduli Idd Amini.
2:Alianzisha vita dhidi ya uhujumu uchumi,biashara ya Ulanguzi,Magendo na aliichukia Rushwa kwa vitendo
3:Alikuwa mzalendo wa kweli wa taifa hili.
4:Aliamni katika siasa na kilimo,akiamini kilimo ni uti wa mgongo wa taifa hii ilipelekea kutotaka kupanda ndege ili ashuhudie juhudi kubwa za Watanganyika katika suala la kilimo
5:Alitunza na kutukuza tamaduni za kiafrika na utaifa wa mtanzania.
Hitimisho, leo ikiwa imepita takribani miaka 30,tangu shujaa wetu na mzalendo hayati Edward Moringe Sokoine tangu atangulie mbele ya haki, je viongozi wetu wa sasa wanaishi na kutenda kwa ajili ya manufaa ya umma kama hayati Sokoine?je?Pengo lake limezibika ama bado?wito wangu kwa wanasiasa wetu nchini wasilitumie jina la kiongozi wetu huyu na baba wa taifa kwa ajili ya kunufaika kisiasa tu?wakati hawamaanishi kwani kuchagua uovu kwenye njia ya haki ni dhambi,na sikuzote ukiwa safarini huwaulizi njia wasafiri wenzako bali wale watokao huko.
(Mungu aipe pumziko la amani nafsi yake na amlaze pema peponi hayati Sokoine)
special thanx kwa
Joseph Moses OleshangayAanyor Engai Ole Lenga na Cosmas Makune
kwa msaada wa baadhi ya taarifa nilizotumia katiaka makala hii maalumu ya kumuenzi Hayati Edward Moringe Sokoine.

FAIDA ZA MATUNDA

FAIDA ZA TANGO
1. Kuzuia kisukari, kuboresha mfumo wa damu na kuondoa kolesteroli mwilini.
2. Chanzo kikubwa cha Vitamin B.
3. Kusaidia kutunza ngozi.
4. Kuongeza maji mwilini.
5. Kukata hangover.
6. Kuimarisha mmeng'enyo wa chakula mwilini.
7. Kuzuia saratani mwilini.
8. Kusaidia kupungua uzito.
9. Kuondoa maumivu na kuboresha viungo vya mwili.
10. Kuondoa harufu mbaya ya kinywa.

FAIDA ZA PAPAI
1. Kuua na kuondoa mazalia ya minyoo mwilini.
2. Kusaidia kutibu vidonda vya tumbo.
3. Kuboresha mmeng’enyo wa chakula.
4. Majani yake huleta ahueni kwa wagonjwa wa saratani.
5. Kupunguza uvimbe (anti-inflammatory).
6. Kuboresha misuli na neva mwilini.
7. Kusaidia kumeng’enya protini.
8. Kuboresha kinga ya mwili.
9. Kuboresha macho.
10. Kuboresha mfumo wa hewa.

FAIDA ZA UBUYU
1. Kuzuia uhalibifu na mikunjo ya ngozi.
2. Kusaidia katika kupunguza uzito wa mwili.
3. Kuimarisha moyo.
4. Kusafisha ini na kuondoa sumu.
5. Kiwango kikubwa cha vitamin C.
6. Chanzo cha madini ya Calcium.
7. Kuimarisha kinga ya mwili.
8. Kuimarisha figo.
9. Kuimarisha mifupa na meno.
10. Kuimarisha mfumo wa fahamu.

FAIDA ZA EMBE
1. Kupunguza kiwango cha asidi mwilini.
2. Kuboresha mmeng’enyo wa chakula.
3. Kurekebisha kiwango cha insulin.
4. Kuboresha macho.
5. Kusafisha damu.
6. Kuboresha ngozi.
7. Kuzuia saratani.
8. Kuimarisha kinga mwilini.
9. Kutibu joto kiharusi (heat stroke).
10. Kupunguza kiwango cha kolesteroli.

FAIDA ZA NANASI
1. Chanzo kikubwa cha vitamin A.
2. Kusaidia kumeng’enya chakula.
3. Inarekebisha mapigo ya moyo.
4. Kuimarisha mifupa ya mwili.
5. Ina kiwango kidogo cha kalori.
6. Inasaidia kuzuia mafua na homa.
7. Kuimarisha mfumo wa kinga.
8. Chanzo cha vitamin C.
9. Inapunguza uvimbe.
10. Kupunguza spidi ya kuzeeka kwa seli mwilini.

FAIDA ZA NJEGERE
1. Kuzuia saratani ya tumbo.
2. Kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu.
3. Chanzo kizuri cha protini.
4. Kuboresha ufanyaji kazi wa ini.
5. Ina kiwango kidogo cha kalori.
6. Kuboresha kinga ya mwili.
7. Inaleta nguvu mwilini.
8. Ina virutubisho vya nyuzi nyuzi.
9. Inazuia kuzeeka haraka.
10. Imejaa virutubishi vingi muhimu mwilini.

FAIDA ZA PILIPILI HOHO
1. Husaidia kupunguza uzito.
2. Kuboresha mzunguko wa damu.
3. Inapunguza kolesteroli mwilini
4. Kuzuia shinikizo la damu.
5. Ina kiwango kidogo cha kalori.
6. Nzuri kwa kuboresha macho.
7. Kuimarisha mfumo wa kinga.
8. Inatibu anemia.
9. Inazua saratani.
10. Kuboresha moyo.

Tuesday, April 05, 2016

DONDOO ZA AFYA NJIA SITA ZA KUNYWA MAJI YA MOTO ZINAZOTIBU MWILI WAKO.


Kunywa kikombe kimoja cha maji ya moto kila asubuhi kinaweza kukutibu mwili wako kwa kusaidia umeng’enywaji wa chakula na kuzuia kuzeeka mapema kabla ya wakati.
Wengi wetu huianza asubuhi vyema kwa kikombe cha kawaha ya moto au chai ya moto kwa lengo la kuuchangamsha miili yetu baada ya kutoka kitandani.
Na pale tunapokunywa maji, basi wengi wetu hupendelea kunywa ya baridi, lakini kwa mujibu wa watalaam wa afya wanatuambia kua tunafanya makosa kufanya hivyo. (kunywa maji baridi)
Mara nyingi unywaji wa maji moto au uvuguvugu, hususani nyakati za asubuhi, inasaidia kuiponya miili yetu na kuitibu pia,
kwa kusaidia kuongeza nguvu katika mmeng’enyo wa chakula ma kupunguza taka mwilini, taka ambazo zinaweza kuzuia kinga zetu kua katika hali yake nzuri ya mfumo sahihi na ambao tunauhitaji.
“matabibu wanasema na kushauri kunywa maji moto ama uvuguvugu nyakati za asubuhi, kila siku, sambamba na mchanyanyo wa maji ya limao, au chai ambayo haina madhara kwa mwili”.
Utumiaji wa maji moto ama vuguvugu huongeza ukazwaji wa utumbo, ambapo husaidia uondoaji wa vitu visivyotakiwa.
Tofauti na maji moto, utumiaji wa maji ya baridi yenyewe huzuia vitu muhimu ikiwemo madini ambayo hua si rafiki kwa mazingira hayo katika mfumo wa umeng’enywaji unapokula chakula.
Kwa wanywaji wa maji ya baridi, inashauriwa kutangulia kunywa maji hayo ya baridi dakika 20 kabla ya kula hata kama maji hayo yanatoka katika vyanzo vya asili vya maji.
Wakati unywaji wa maji ya moto ama vuguvugu yanaweza yasiwe mazuri kwa ladha yanapokua mdomoni,
Hizi hapa zifuatazo ni sababu kwanini tunywe maji ya uvuguvugu;

1. Hurahisisha umeng’enywaji wa chakula.

Maji ya moto ama vuguvugu katika kikombe uamkapo asubuhi yanaweza kuusaidia mwili wako kutoa nje sumu katika mwili.
Maji na vimiminika vingine husaidia kuvunja vunja chakula katika tumbo na kuweka mfumo wa chakula kuwa katika hali nzuri ndani ya mwili. Maji moto au vuguvugu husaidia kuweza kuvunja vunja chakula hicho kwa uharaka zaidi, na hivyo umeng’enywaji wa chakula kua mwepesi na wa haraka.

2. Unywaji wa maji ya baridi wakati ama baada ya mlo.
Unywaji wa maji baridi wakati au baada ya mlo wako unaweza kusababisha kusaidia kugandishwa kwa mafuta ambayo unayapata kupitia chakula, na hivyo kusababisha mrundikano wa mafuta katika utumbo.
Uongezwaji wa barafu ili kutengeneza maji ya baridi hufanya kubadili mfumo halisi wa madini na virutubisho katika mwili ambavyo madini hayo ni muhimu katika kuuweka mfumo wa chakula katika hali ya afya, ambapo pia unaweza kufanya njia mbadala kwa kunywa chupa ya maji ya baridi sambamba na chupa ama glasi ya maji ya uvuguvu au moto ili kusaidia umeng’enywaji wa chakula, hususani baada ya kula chakula chako.

3. Husaidia kulainisha choo
Kwa pointi moja au nyingine, wengi wetu tunakabiliwa na vidonda hususani matatizo ya tumbo ambapo hua na choo kidogo au kukosa kabisa haja kubwa.
Vile vile ugumu wa haja uendapo msalani wakati wa kukitoa, husababisha kuchanika au kuchubuka katika sehemu ya kupitia haja kubwa,
Haya yote yanaletwa na ukosefu wa maji mwilini.
Unywaji wa maji moto au vuguvugu nyakati za asubuhi wakati tumbo likiwa halina kitu unaweza kusaidia utumbo mpana kusukuma uchafu/ kinyesi vizyri na kusaidia kuwa na choo laini {kinyesi chepesi} wakati wa uvunjwaji wa chakula na hata usafirishwaji wake hua mzuri kupita utumbo.
Hivyo uchangamshwaji wa utumbo na maji moto husaidia kuurudisha mwili katika ufanyaji wake mzuri na wakawaida wa kazi vyema.

3. Huondoa maumivu
Maji ya moto au vuguvugu, tukizingatia ni maji asilia ambayo wengi wetu katika majumba hutumia, husaidia kuondoa maumivu ya tumbo la hedhi kwa wakina mama na maumivu ya kichwa.
Umotomoto toka kwenye maji moto huweza kua na athari chanya katika misuli ya tumbo, ambapo huweza kusaidia kuondoa papo kwa papo makazo na misuli kujinyoosha.
Kwa mujibu wa Healthline, wanasema maji moto au vuguvugu ni mazuri kwa maumivu, ambapo kimiminika hicho cha moto huongeza mzunguko wa damu kwenye ngozi na kusaidia kushusha maumivu ya misuli.

4. Husaidia kupunguza uzito
Kama uko katika mlo wako, unywaji wa maji nyakati za asubuhi basi unaweza kukusaidia katika kupunguza uzito.
Maji moto ama uvuguvugu husaidia kuongeza joto la mwili, ambapo huongeza metabolic/ kiwango cha ufanisi wa kazi katika mwili.
Kadri kiwango cha ufanisi wa kazi katika mwili kinapoongezeka huuruhusu mwili kuchoma kalori nyingi katika mwili.
Hivyo husaidia figo na gastro intestinal kufanya kazi zake vizuri mwilini.
“madaktari wanashauri kua unywaji wa maji moto nyakati za asubuhi, kila siku, pamoja na limao ndani yake, au chai huondoa vitu hatari mwilini”.
Unywaji wa glasi kadhaa za maji moto au vuguvugu na limao ndani yake husaidia kuvunjavuja tisu za mafuta katika mwili na husaidia mmeng’enyo wa chakula.

5. Kuboresha mzunguko wa damu
Mrundikano wa mafuta katika mwili huondolewa wakati wa unywaji wa maji ya moto.
Hii husaidia kuondoa sumu ambazo hua zimezunguka katika miili yetu kwa kufanikisha mzunguko wa damu.

6. Hupunguza hatari ya kuzeeka mapema
Hii inaweza kuzuilika kwa kunywa maji moto ama vuguvugu, upatikanaji wa sumu katika mwili hupelekea kuzeeka mapema na kwa haraka, lakini maji moto ama vuguvugu YAnaweza kusaidia kusafisha mwili kwa kutoa sumu mwilini, hata hivyo pia kuirekebisha ngozi kwa kuoneza SelI mpya maeneo ya ngozi.
Medical Daily linasema kua “wanawake siku zote hunufaika kwa sababu wanakua na homoni nyingi zaidi ambazo huhusika na maji moto,”
Kuweza kua ama kuongeza uimara wa afya yako kupitia unywaji wa maji moto ama vuguvugu, kunywa kila siku asubuhi maji pekee au yaliyochanganywa na limao kwa kuyapa ladha.
Wanywaji wa maji vuguvugu au moto kwa, kadiri wanavyokunywa maji hayo wanaweza kua wanaangamiza tisu za mdomoni na hata maeneo ya koromeo.
Baada ya kuunguzwa na maji hayo ya moto,
Basi huna budi kuyaacha yapoe kidogo kabla ya kuanza kuyatumia kwa kuyanywa.
Vile vile inashauriwa “ kila mara umuone daktari kwa maelezo kabla ya kuanza kunywa maji hayo ya moto, kama utakua katika matumizi mengine ya dawa, ambazo zinaweza kuleta madhara katika ufanisi wa dawa husika.