Monday, March 25, 2013

MWANAUME KWA MWANAMKE!


  Kila msichana inampasa awe na muda nyeti wa kutafakari.  Je, unataka kuolewa na kisha upewe talaka?  Katiba mpya ya Wazimbabwe ina uwezekano mkubwa wa kuhalalisha mitala iwapo michango ya mawazo kutoka kwa WAMANICALAND itakubalika. Je, unaweza kuvumilia ndoa ya mitala?  Unataka mwanaume anayesema, “nililipa mahari hivyo inakupasa ufanye kama ninavyotaka la sivyo”
     Hakuna mtu kwa akili zake timamu atajiingiza katika uhusiano usio na thamani hivi. Swali la kujiuliza ni “Kwa vipi, nitazuia uhusiano wa namna hii”? Kabla hatujakwambia ni kwa vipi, ni kukuelezea kuhusu vijana wane ambao una uwezekano  wa kukutana nao. Mwanafalsafa aliyeitwa Hippocrates alikuwa wa kwanza kuwaweka watu katika makundi manne.  Makundi hayo manne yalijulikana  kama “TEMPERAMENTS ,” “Temperament” linatoka katika lugha ya kilatini  na lina maana ya kuchanganya vitu vya maji maji  na hasa vitu vya maji maji ya mwili.  Majina manne yalimjia mawazoni ambayo ni Sanguine, Choleric, Melacholy na Phlegmatic.

 Mr. Sanguine/Bwana mtazamia mema tu:,
     Mtu huyu ana chembechembe nyekundu nyingi mwilini zinazokimbiakimbia ndani ya mishipa ya damu. Ana msisimko mkubwa wa maisha, Ukimkuta kwenye sherehe, wakati wote utakuta amezungukwa na umati wa watu. Anapotoa hadithi, kila mmoja anaacha alilokuwa akifanya na anamsikiliza kwa makini. Haina haja kusema, anafahamika na watu wengi. Wasichana wanamgombania kuliko mwingine yoyote kama utatembea naye utapata msaada wowote unaohitaji lakini hawawezi kufanya uamuzi ni lini atakuoa. Ni aina ya mtu yule ambaye ni vigumu mikono yake kukaa mbali na Matiti au sehemu nyingine nyeti za viungo vya mwili wako.
    Mr. Sanguine kwa kawaida ni msahaulifu sana na hana mpangilio. Huchelewa kila wakati katika mipango yake kwa vile anakuwa akiburudisha watu. Katika wingi wa maneno kuna dhambi. Ataishiwa na habari za kweli na ataingilia kusema visivyo.

Majaribu:
     Ukiwa una mapenzi na mtu kama huyu, una haja ya kuelewa hili, Anajaribiwa anapokuwa hajaliwi na kuhakikishiwa kukubalika. Mtu huyu anakuwa si salama kwa jinsia tofauti kwa vile anapenda matembezi na kusikilizwa. Anavutiwa na wasichana ambao wanafikiria kwa kina na atamwoa msichana wa namna hii ili kufidia mapungufu ya haraka zake na mipangilio.

Mr. Choleric/Bwana Chuki.
       Mtu huyu ana nyongo ya manjano nyingi ambayo humfanya awe mgomvi Na mwepesi wa hasira. Ni mtu wa vitendo. Kama unapenda michezo ya kuigiza ya “Rambo au Texas Ranger” basi hayuko mbali na waigizaji hawa.



Majaribu:
       Kama utakuwa umempenda mtu wa namna hii, uelewe kuwa anaweza kujaribiwa na wanawake wengine kama hutaonyesha kuridhika au kukubali analolifanya. Wanawake
wengi humdharau kwa maana anataka ashikilie kila kitu yeye mwenyewe.  Huenda umekutana na kijana huyu kanisani.  Ni mhubiri mkuu, ambaye anajitolea muda wake mwingi kujishughulisha na programu za vyama vya vijana/wazee na utoaji wa neon la Mungu ambapo hufikiria kuwa ndio yenye thamani. Lakini ni mara nyingi hana rafiki wa kike.  Anavutiwa na wanawake ambao humkubali kwa sababu anampa nafasi ya kutawala.  Wanawake wenye malengo madhubuti maishani au apendaye michezo atapata shida sana akitembea na mtu wa tabia hii.

Mr. Phlegmatic/Bwana Mtulivu.
    Kijana huyu ni mwenda pole kwa kila alifanyalo.  Ni mtulivu, mwenye subira na aliyejitayarisha.  Anawakilisha mawazo ya watu wengi walio Wakristo/Waislamu. Ni mara chache kugombana na mtu yeyote na husikiliza wakati wengine wanapoongea. Huwa hana mengi ya kusema, ila ni mwingi wa maneno ya ucheshi.  Ili mradi watu hawamshambulii kwa lolote, atakuwa na furaha.  Anapenda kulala masaa mengi kuliko vijana wengine wote.  Katika maisha yake ya utu uzima anaweza kuwa na kitambi.

Majaribu:
      Bwana huyu anataka kuheshimika tu.  Mara anapoanza kujiuliza umashuhuri wake, anajisikia kushindwa na mtu anayempa mawazo mazuri.  Huenda umekutana na mtu huyu Kanisani/Msikitini au Popote.  Ni kijana ambaye atamwomba msichana wawe wachumba na hatakama atasema hapana, atamsubiri hata miaka 2 hadi 3 ili abadili mawazo.
      Mtu huyu ni mara chache kutoa hati ya talaka.  Lakini kwa vile Bwana Mtulivu kwa kawaida huoa mwanamke mwenye uwezo wa kujitetea na mwenye msimamo, mwanamke kwa kawaida ndiye hutoa talaka..


Mr. Melancholy/Bwana Mchungu.
      Kijana huyu hutegemewa kuwa ana mchanganyiko wa “melas” kwa Kigiriki Nyeusi na “chole” au nyongo.  Yeye ni mwepesi kuwa na msongo wa mawazo na kukata tamaa. Yeye ni Bwana “Mkamilifu” na anafuatilia mambo kwa undani ambao wakati mwingine hukasirisha wengi.  Kwa kawaida ni mwenye uwezo wa akili wa kuchanganua kila kitu.  Wanamuziki na hasa wale ambao hutunga nyimbo zao wenyewe huangukia kwenye kundi hili.  Mtu wa kundi hili ana tabia isiyotabirika.  Anaweza akafurahi sana dakika moja (1), na akawa amehuzunika sana saa moja(1) baadae.

Majaribu:
      Ikiwa wewe ni rafiki wa Bwana Mchungu elewa kwamba anajaribiwa wakati usipojali kuelewa mahitaji yake kwa undani.. Kwa vile yeye ni mnyazifu na ni mfuatiliaji mzuri wa warembo wanaopenda kutembeatembea, ni mara nyingi huepuka kujizamisha kwenye uhusiano wa kuzeeshana na badala yake hujizamisha katika vipawa walivyo navyo.

Mvuto wa Jinsia Tofauti:
       Watu wa asili huvutiwa na mtu ambaye unyonge wake ndio nguvu yao na kinyume chake.  Mungu alichompangia au kumchagulia mtu ndicho kilicho chema kwetu.  Umeshangaa kwa nini wasichana walio wa kiroho huvutiwa na wavulana wa kiulimwengu?

Nitahakikishaje naolewa na bwana shihi?
        Katika kitabu cha Alberta Mataz kijulikanacho kama “Caliphate with love” hufanya mapendekezo imara ambayo hata sisi tunayapendekeza.

OMBA:
         Unahitaji kutumia magoti yako mapema maishani. Kabla kabisa hujaanza kuchumbia au kuchumbiwa inakupasa uombe kupata Ndoa yenye furaha. Kama usipomshirikisha Mungu katika kutafuta ndoa yenye furaha, kuna uwezekano kuwa utakuwa unafukuzana na upepo tu. Usianze kuwa mcha Mungu ati kwa sababu unataka mtu wa kuoa au kukuoa. Hakikisha kuwa una uhusiano wa muda mrefu katika maisha yako na Mungu. Hazipo hasara yoyote kwa dondoo hii, kama utafaulu katika sehemu hii mengine yote hufuata mtiririko kwa urahisi  katika nafasi yake.  Yesu anasema; “Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni nanyi mtapewa/mtapata furaha yenu iwe timilifu. Mimi nalikuja ili wawe na uzima, kasha wawe nao tele” Yohana 16:24; 10:10

Epuka Ngono kabla ya Ndoa:
      Kila mvulana mkristo/Muislam mzuri hutegemea kuoa Bikira. Hata wale ambao sio Mabikira wenyewe wanapendelea kuoa Bikira. Mwanamke huwa na hasara zaidi kuliko mwanaume kama mambo yakienda kombo. Akipata mimba, anaacha shule/chuo kusoma; na watu humbatiza majina. Kama ulidanganywa au kwa hiari yako mwenyewe ulikubali kupoteza Ubikira wako, inakubidi ufikirie nafasi nyingine kwa kuacha ngono na kutafuta ubikira wa awamu ya pili.
       Kusudia kuutunza mwili wako kwa ajili ya mume atakayekuoa. Vijana wa kiume wengi wanaweza kuvumilia msichana ametubu njia zake mbaya za kwanza. Pia jifunze kujisamehe, wakati Mungu anaposamehe, anakusamehe kabisa. Hahitaji kufufua dhambi zako wakati wa hukumu ili akuhesabie hatia. Mshahara wa dhambi ni umauti. Je ingekuwa kurudia kitendo hiki ningerudia? Kama jibu ni hapana,basi acha kujihukumu.

Wazazi wahusishwe.
       “Kama umebarikiwa kuwa na wazazi wacha Mungu omba ushauri wao.  Waambie matumaini na mipango yako. Jifunze mafundisho waliyoyapata na kujifunza katika uzoefu wa maisha yao, mara nyingi yatakuepusha kuumia roho,”  Dondoo hii imetolewa kwa (Messages to young people) na Ellen G. White. Hii ni kwa vile wasichana wengi huanza kuchumbiwa wakati wa kubalehe mapema kabla wazazi hawajategemea kuwa wangefanya hivyo.  Wanajikuta wanakamatwa bila kujijua.
        Husisha watu wa kundi la vijana wenzako katika kila uhusiano unaojiingiza kwao (Makundi mema).  Haya yatakusaidia wakati utakapojaribiwa. Kadiri unavyoudhi watu wengi kwa uamuzi wako mbovu, ndivyo utakavyokuwa na nafasi chache za kupanga ngono kabla ya ndoa.
         Wakati mzuri wa kuwa na mahusiano ya mtu na mtu ni baada ya kumaliza masomo ya shule ya Sekondari. Jihusishe na kazi katika makundi kama huhitaji kuwa na tabia ya bandia.  Jiwekee lengo la kuwa na tabia nzuri bila kujilinganisha na mtu mwingine. Hutakuwa na maudhi mengi.

Mwishoni.
       Jaribu kuachana na vijana wa kiume ambao hawana mwelekeo katika maisha yao. Achana na vijana wa kiume wenye msisimko, wasiojizuia na wasio na afya kihisia.  Vinginevyo utaishia kuwa mama watoto wao. Vijana ambao wana aibu sana, wakaidi, wenye kushuku, wenye kugawa fedha zao ovyo ili kuwafurahisa wengine, wenye hasira ambao kila wakati wanazungumzia ngono, waongo ili kuwafanya waonekane bora na wale ambao wanakutegemea kwa kila jambo.  Vyote hivyo sio vizuri katika ndoa, usijihusishe nao, Jielimishe kuwa unataka nini kutoka kwa jinsia tofauti……’Smart love” uk. 235-236 na Nancy Pelt.
       Usisahau kuwa Kama mwanamke unaweza kudhurika zaidi kwa mapendekezo kuliko wanaume walivyo. Kama hawa unaweza kudanganywa kwa ahadi za wanaume wanaozungumza kwa unyenyekevu. Lakini usifanye uamuzi wote wa msingi wa unavyojisikia, fikiria kila kitu Mungu anaweza kukusaidia kuwa mwanamke bora zaidi.

                                                                                               Created by Michael Nyagei Magessa

0 comments:

Post a Comment